Dawa za kuzuia ubalehe ni homoni zinazotolewa kwa watoto ili kuchelewesha ubalehe wao.
Dawa hizo zilianza kutumika katika miaka ya 1980 kwa watoto walioanza mapema mno kubalehe, lakini baadaye zilianza kutumika kwa wale wasiojisikia vizuri katika jinsi yao ya kuzaliwa, kwa kawaida ili kurahisisha baadaye upasuaji wa kuwalinganisha na jinsia waliojichagulia.
Kadiri kesi hizo zinavyoongezeka, wanazidi kupatikana wanaojuta hatua walizochukua kujibadilisha[1][2][3] na wanaolaumu waliowashauri vibaya [4][5][6][7][8].
Wanafanya hivyo hasa wale waliopewa haraka [9][10][11][12] dawa hizo [13][14] na hatimaye kufanyiwa upasuaji [15][16] kabla hajaweza kuelewa matokeo yake [17][18][19][20] bila kuzingatia njia mbadala[21].
Baadhi ya waliojuta wamefungua kesi dhidi ya waliowaelekeza [22][23][24], hasa baada ya kuona ugumu mkubwa wa kurudia hali asili (jambo ambalo pengine haliwezekani kabisa, hasa upande wa uzazi)[25][26].
Baadhi wanafikia hatua ya kujiua [27][28][29].
Hatua zao hizo, pamoja na hoja za wataalamu mbalimbali zinazoeleza madhara ya dawa hizo, zimelazimisha wenye mamlaka katika nchi mbalimbali kuchukua uamuzi wa kusimamisha mchakato wa namna hiyo [30][31][32][33][34][35][36][37][38][39][40].
Kati ya utafiti uliofanywa kuhusu taratibu zilizotumika miaka ya mwisho, ripoti ya Uingereza maarufu kama imefanya serikali yake isimamishe matumizi ya dawa hizo kwa watoto[41] ikifuata zile za Uswidi na Ujerumani.
© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search